|
mtoto anety akionesha jeraha alilounguzwa na mama yake |
|
mama ambaye jina lake halikufahamika akiwa amembeba mtoto tayari kwa kumpeleka hospitalini |
MTOTO aliyejulikana kwa jina moja la Aneth (pichani) anayekadiriwa kuwa
na umri wa miaka miwili, mkazi wa eneo la Majengo Kaskazini jijini Mbeya
ameunguzwa vibaya mwili wake na kulazimishwa kula kinyesi na Mama yake
Mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Revina.
Tukio hilo la
kikatili liligundulika jana eneo hilo majira ya saa tano asubuhi ambapo
mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio na kuukuta umati wa watu
na mtuhumiwa akimuogesha mtoto huyo.
Mtoto huyo alipoulizwa kuwa ilikuwaje, aliongea kwa woga akisema kuwa alikuwa amefungwa mkono na kumwagiwa maji na kupigwa.
Mtuhumiwa
huyo alipohojiwa alikataa kusema chochote na kuishia kutaja jina lake
moja la Revina, kisha wananchi wakaamua kumchukua mtoto huyo na
mtuhumiwa na kuwapeleka kituo cha Polisi cha Kati.
Mashuhuda wa
tukio hilo walisema kuwa baada ya kutomuona mtoto huyo mwenye historia
ya kuteswa na mama yake huyo mdogo anayeelezwa kuwa mama yake mzazi,
Bahati Mkandara alifariki, wakaamua kumuuliza binti huyo ambapo
aliwajibu kuwa mtoto huyo alikuwa kucheza na walipompiga ndipo akaamua
kukimbilia chumbani na walipoingia wakamkuta mtoto amesimama akiwa uchi.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Kaskazini, Shack
Mwakanyamale alisema kuwa binti huyo amezoea kumtesa mtoto huyo huku
mtoto wake akiwa na afya njema ambapo aliwatuliza wananchi wenye hasira
kali na kuongoza msafara wa kumpeleka katika kituo cha polisi mtuhumiwa
huyo