![]() |
| Kamanda wa polisi mkoa wa iringa. |
Mtu mmoja amefariki dunia kwa kupigwa na radi wakati akichunga ng’ombe
katika kijiji cha kibena Wilaya ya Iringa vijijini.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani IRINGA ACP
RAMADHAN MUNGI amesema mtu huyo alietambulika kwa jina la ZAKARIA KIBUGA
alifariki papo hapo baada ya kupigwa na radi hapo jana majira ya saa 10 jioni.
Aidha radi hilo pia limesababisha vifo vya ng’ombe 22 wenye thamani ya
shilingi milioni 44 mali kampuni ya EFAS FARM LIMITED.




0 comments:
Post a Comment