Hatimaye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika Urusi kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Algeria Mbweha wa Jangwani ndio umechezwa leo November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, mchezo wa marudiano utachezwa November 17 Algiers.
Takwimu za mchezo huo zilikuwa rafiki
kwa upande wa timu zote mbili kwani kabla ya kupigwa mchezo huo, kwa
takwimu za hivi karibuni Taifa Stars iliwahi kucheza na Algeria September 3 2010 Algiers na kutoka 0-0 katika mchezo wa AFCON, lakini September 3 2011 Dar Es Salaam Stars ilitoka sare ya goli 1-1 kitu ambacho kilifanya timu zote kuwa na rekodi ambazo haziwezi kumtisha mwenzake.
Kipindi cha pili Taifa Stars walirudi kwa kasi na Mbwana Samatta
akadhihirisha ubora wake wa kupachika magoli baada ya dakika 54
kupachika goli la pili kwa Stars, furaha ya watanzania ilianza kupotea
dakika ya 71 Sliman Islam alipachika goli la kwanza la Algeria na dakika
mbili mbele akapachika goli la pili, hadi dakika 90 zinamalizika Taifa
Stars 2-2 Algeria.





0 comments:
Post a Comment